Saturday, April 10, 2010

Tuangalie Miongozo ya Teknohama

Unapoona maelezo Fulani kuhusu programu kwenye mtandao ukaipenda ukaamua kuitumia kwenye kompyuta yako hapo kazini bila kuwasiliana na msimamizi wa masuala ya teknohama mahala hapo hilo linaweza kuwa kosa chochote kinaweza kutokea baada ya wewe kutumia program hiyo .

Wakati mwingine unaweza kuamua kuita mtu wa nje ya ofisi yako kuja kufanya kazi Fulani kwenye komputa ambayo ni mali ya ofisi unayofanyia kazi bila mawasiliano ya wana teknohama au watu wengine wa eneo hilo hilo nalo ni kosa , mfano data zaweza kuibiwa au kuhamishwa au kuharibiwa .

Hata jinsi unavyoshiriki kwenye baadhi ya majukwaa kwa njia ya mtandao hili nalo ni kosa kwa namna moja au nyingine lakini hiyo zaidi inategemeana na shuguli za kampuni au sehemu unayofanyia kazi , unatakiwa uongee kwa maslahi ya kampuni unayofanyia kazi kwenye kutoa maoni au ufafanuzi Fulani

Sio kushiriki tu kwenye majukwaa hayo hata unavyoamua kwa makusudi kabisa kuweka picha zako na taarifa zako zingine kwenye mitandao mbalimbali ya marafiki na ukaacha watu watoe maoni yao kuhusu picha na taarifa zako zingine hili nalo laweza kuwakosa ila unaweza kuona baada ya siku nyingi .

Mwaka jana kuna mama mmoja alitoa taarifa anaumwa kazini kwake kwahiyo akawa mapumziko kwenye mapumziko hayo akapiga picha ambazo aliweka kwenye mtandao wake ambapo mmoja wa makuu wake wa kazi aliona anafuraha na yuko kwenye starehe kwahiyo alisimamishwa kazi huyo mama .

Vitu vyote hivyo nilivyotaja hapo juu havijulikani na watu wengi sana wanaofanya kazi kwa kutumia kompyuta au kuhusisha kompyuta kwenye maofisi na sehemu zao zingine za kazi na tatizo kubwa limeonekana ni miongozo ambayo kwenye ofisi hizo hakuna au ipo lakini haifuatiliwi kuhakikisha inafanya kazi ipasavyo .

Katika miongozo hii ya matumizi ya kompyuta na vifaa vyake iko ya aina karibu 3 ingawa yote inaweza kuwa chini ya muongozo mmoja wa nchi yote mfano mzuri tumeona miongozo ya nchi kama uchina ambapo imesababisha kampuni la google kuamua kuondoa huduma zake huko kwa kuzipitishia nchi ya hong kong .

Aina hii ya miongozo kwanza ni ule unaohusu nchi nzima pale inapotakiwa kuwa na muongozo wake ambapo utakuwa supported sana na sheria za mitandao kwahiyo kampuni na mashirika ya umma yanapokuwa na miongozo yao inabidi kutumia baadhi ya vifungu kwenye muongozo wa taifa pamoja na sheria za mitandao .

Pili ni miongozo ya wizara na shuguli zingine za kiserikali ambazo ziko kwa maslahi ya serikali na idara zake kadhaa haswa za mambo ya ndani na nje hapo ndipo tunapoona mfano wa kwanini google waliamua kuhamisha huduma zake toka uchina kupitishia hong kong .

Tatu ni miongozo inayohusu sekta binafsi ambapo kuna kampuni kadhaa haswa zile zinazohusu mawasiliano au huduma zingine za mawasiliano hapa kuna mambo kama ya kuhifadhi taarifa za mteja wa huduma za mawasiliano kwa kipindi Fulani kwa ajili ya kodi na mambo mengine ya kisheria , kampuni zote za kigeni zinazowekeza nchini na kuamua kutumia huduma za mawasiliano inabidi kusoma miongozo hii na kuhakikisha inafuatiliwa kwa karibu zaidi .

Nchi yoyote inayokuwa na miongozo ambayo ni dhaifu inachangia sana katika uhalifu unaohusu mitandaona aina zingine mbalimbali za hujuma ndani na nje ya nchi hiyo tumeona nchi ya Nigeria kwa kushirikiana na taasisi zao kadhaa zilivyoamua kuimarisha mifumo yake ya mitandao na kuweka miongozo hiyo matokeo yake ni kwa wahalifu wa kimtandao wan chi hiyo kutumia nchi jirani ambazo hazina sheria kali kwa ajili ya kuendesha uhalifu huo .

Taarifa za uhalifu wa mtandao kuanzia mwaka jana na mwanzoni mwa mwaka huu zinaonyesha kwenye nchi kama afrika ya kusini uhalifu umeongezeka sana wa mtandao nchi hii ina sheria dhaifu za mitandao na miongozo matokeo yake ni wahalifu wa sehemu zingine kutumia mwanya huo kuendesha hujuma zao .

Hapa kwetu hatujachelewa sana watu wengi wanaongezeka katika kutumia mitandao na huduma zingine mbalimbali sasa kunahitajika miongozo hii ieleweke kwa watu mbalimbali kunahitajika sheria kali na kunahitajika elimu zaidi kwa watu wetu kwenye masuala ya ulinzi na usalama ili huko mbeleni tusije juta bure .

0 comments:

Post a Comment